AUNTY EZEKIEL ASEMA HAKUNA WA KUWATENGANISHA NA MOZE IYOBO

STAA wa kike wa filamu nchini, Aunty Ezekiel amesema uimara wa mapenzi kati  yake na baba wa mwanaye, Moze Iyobo ndiyo chanzo cha watu kupenda kumsakama mara kwa mara.

Hata hivyo alisema kuwa watu hao hawatafanikiwa kuwatenganisha na zaidi wanachangia kuongeza uimara wa penzi hilo ambalo sasa limezaa matunda kwa kupata mtot0 mmoja.


“Nilishawahi kuwaambia kwamba kama kuna mwanamke ambaye ana cheti cha ndoa na Mzee Iyobo ajitokeze vinginevyo siwezi kuachana naye hadi sasa hakuna aliyejitokeza wamebaki kunisema tu."

No comments