AUNTY EZEKIEL: SIJIPENDEKEZI KWA ZARI, NI BOSI WA MKATA VIUNO WANGU

MSANII wa filamu, Aunty Ezekiel ameonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya watu kudai kwamba anajipendekeza kwa Zari ilihali ni rafiki wa Wema Sepetu, ambapo aliema anafanya atakalo bila kuingiliwa na mtu.

“Nataka niwaambie kitu kimoja, maana kumjibu mmoja mmoja muda huo sina… ninafanya nitakalo sifanyi mtakayo maana nina hakika nyie mnaoka kubishana na mimi vibanda vya mbavu za mbwa vinawashinda, hivyo muda mnaokaa kufuatilia yangu mngeenda kutafuta ya kufanya,” alisema Aunty Ezekiel.

“Mnataka nibadili nyekundu kuwa njano, kwani yule si ni bosi wa mkata viuno wangu? Sasa kama ni bosi mlitaka nibishe niseme mimi ndio bosi, basi nifungue bendi yetu acheze!” Aunty Ezekiel aliandika katika Instagram.


Hivi karibuni mwigizaji huyo aliyezaa na dansa wa Diamond Plutnamz, Moze Iyobo, alionekana akila bata kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Zari ambaye ni mpenzi wa Diamond, licha ya kufahamika vyema kuwa ni shosti wa karibu wa Wema, mpenzi wa zamani wa supastaa huyo wa Bongofleva.

No comments