BABY MADAHA ASEMA WANAUME WA KIBONGO WABABAISHAJI KATIKA MAPENZI

STAA wa muziki wa Kizazi Kipya Baby Madaha ametoa sababu amnbazo zimemfanya aamue kupata mchumba kutoka nje akidai kwamba wanaume wa Tanzania ni wababaishi hawana mapenzi ya dhati.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ameamua kuhamishia moyo wake kwa mataifa mengine kutokana na kile anachoamimi mtu wa nje anapoamua kupenda huwa hana mzaha.

“Sitaki wanaume Watanzania kwa sababu wengi wao sio wakweli hawana mapenzi ya dhati na sasa nimehamishia moyo wangu kwa mataifa mengine,” alisema.


Kwa muda mrefu kimwana huyo amekuwa akisema kuwa ana mchumba wake wa Kiarabu anayeishi naye huko Umangani hali inayomfanyaaishi nchi mbili kwa nyakati tofauti.

No comments