BALOTELLI AMFICHUA JURGEN KLOPP AKISEMA WALIKUWA "HAZIIVI" LIVERPOOL

KWA lugha nyingine unaweza kusema ni kama kampotezea baada ya straika Mario Balotelli kusema kwamba hana uhusiano mzuri na kocha wake Jurgen Klopp ambaye alimwambia aondoke Liverpool ili akacheze kwa mkopo katika timu nyingine.

Muitaliano huyo alisajiliwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Brendan Rodhgers mwaka 2015 akitokea AC Milani lakini akashindwa kutamba akiwa na Reds kabla ya kurejeshwa Rossoneri kwa mkataba wa muda.

Na kwa sasa staa huyo anakipiga katika timu ya Nice ambako ameshafunga mabao sita katika mechi tano za kwanza baada ya kuondoka Liverpool akiwa mchezaji huru mwishoni mwa dirisha la usajili majira haya ya joto.


Kwa sasa Balotelli ameamua kuweka wazi akisema kwamba hakuna nafasi yoyote ya kurejea katika klabu ya Anfield baada ya kushindwa kuelewana na Klopp.

No comments