BARAKA DA PRINCE ALALAMIKA KUBEZWA RANGI YAKE NA STAN BAKORA

NYOTA wa Bongofleva nchini, Baraka Da Pince amemjia juu na kumlalamikia msanii mwenzake, Stan Bakora kwa kitendo cha kuikashifu rangi yake ya asili.

“Ameniudhi sana Stan Bakora, napenda sana rangi yangu na ndiyo maana mimi si kama wasanii wengine ambao wakishatoka kimuziki hubadili rangi zao, mimi ni mweusi na nitazidi kuwa mweusi ila alichokifanya Bakora ni kunidhalilisha," alisema Da Pince.

Stan Bakora ameurudia wimbo mpya wa Baraka Da Pience uitwao "Bado" na katika video anaonekana akiwa mweusi tii ikimaanisha Baraka anafanana hivyo.


Kwa upande wake, Stan anasema kuwa yeye ni msanii wa vichekesho hivyo alipaswa kufanya vile ili mtu akitaza video hiyo asiishiwe na hamu ya kuitazama mara kwa mara.

No comments