BARCELONA HATARINI KUWAKOSA WALINZI JORDI ALBA, GERARD PIGUE

TIMU ya Barcelona huenda ikawakosa wachezaji wake muhimu katika safu ya ulinzi Jordi Alba na Gerard Pique katika mechi mbili zajazo baada ya kutolewa uwanjani katika mchezo wa Ligi ya mabingwa ambao waliibuka na ushindi mnono dhidiya Manchester City.

Hali hiyo kutokana na kwamba mastaa hao wawili wa timu ya taifa ya Hispania walitolewa nje ya uwanja kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia jana ambao timu yao iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 na nafasi zao zikichukuliwa na Lucas Digne na Jeremy Methieu.

Baada yua mchezo huo Barca ilieleza kuwa beki wa kushoto Alba alikumbana na matatizo ya misuli ya nyama za paja na Pique anasumbuliwa na matatizo ya enka.


“Majeraha Gerard Pique na Jord Alba ambaso wote walipumzishwa katika mchezo ambao Barca waliibuka na ushindi dhidi ya Manchester City kwenye uwanja wa Nou Camp litakiuwa pigo katika safu ya ulinzi ya Luis Enrique,” ilieleza ctaarifa yta klabu hiyo.

No comments