BEKI DJBRIL SIDIBE WA UFARANSA "AIKONDEA" LIGI KUU ENGLAND

BEKI wa timu ya taifa Ufaransa, Djibril Sidibe amesema kuwa alitaka kujiunga na Arsenal dakika za mwisho za usajili msimu uliopita na badala yake akaenda kujiunga na Monaco lakini akasema kuwa bado anatamani kucheza kwenye michuano ya Ligi Kuu England.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Monaco akitokea katika timu ya Lille Julai, mwaka huu ambako alikuwa ameshaitumikia klabu hiyo kwa misimu minne.

Hata hivyo Sidibe kazungumza jinsi alivyokuwa njiapanda wakati Arsenal walipomfuata muda mfupi kabla ya kukamilisha usajili wake akisema kuwa uamuzi wake ulitojana na kuwa alikuwa akitafuta muda mfupi kabla ya kukamilisha usajili wake.


“Nilikuwa njiapanda kukamilisha usajili na Arsenal wakiniongezea msongo wa mawazo wakati waliponifuata dakika za mwisho,” alisema staa huyo.

No comments