Habari

BENTEKE AWEKA REKODI MPYA KOMBE LA DUNIA WAKATI UBELGIJI IKIUA 6-0

on

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool Christian Benteke ameweka rekodi mpya kwa kufunga goli la mapema zaidi katika historia ya Kombe la dunia.
Benteke amefanya hivyo katika mchezo wa kundi H wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia kati ya nchi yake ya Ubelgiji dhidi ya Gibraltar.
Wakati Ubelgiji ikivuna ushindi mnono wa bao 6-0, ni Benteke aliyekuwa gumzo baada ya kufunga goli la kwanza kunako sekunde ya saba.
Bao hilo la Benteke anayeichezea Crystal Palace ya England, linafuta rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Davide Gualtieri  wa San Marino aliyefunga goli la sekunde ya nane mwaka 1993 dhidi ya England.   
Belgium striker Christian Benteke scored the fastest ever goal in World Cup history
Mshambuliaji Christian Benteke amefunga goli la mapema zaidi katika historia ya World Cup 
TV footage shows six seconds on the clock but the goal was officially clocked a second later
Ni bao la sekunde ya 6 kuelekea sekunde ya 7

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *