BRENDAN RODGERS ATABIRI MOUSSA DEMBELE KUJA KUWA KAMA DIDIER DROGBA

KOCHA wa Celtic, Brendan Rodgers amesema staa wake Moussa Dembele anaweza kufikia mafanikio ya straika wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba.

Dembele mwenye umri wa miaka 20, ameanza vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mara mbili kwenye mchezo wao dhidi ya Manchester City ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 3-3.

Rodgers alisema kuwa anaamini mshambuliaji huyo ana uwezo wa kufikia kiwango cha Drogba ambaye alifanya makubwa akiwa na Chelsea.


“Hakuna mashaka kuhusu hili, nimewahi kufanya kazi na Didier nikiwa Chelsea na ninafikiri Moussa ana uwezo unaofanana na wake,” alisema Rodgers.

No comments