CHRIS SUTTON ATAKA WACHEZAJI WANAOUNGA MKONO MAPENZI YA JINSIA MOJA WARUHUSIWE KUJITANGAZA

ALIYEKUWA mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa katika Ligi ya Uingereza, Chris Sutton amesema kuwa wakati umefika kwa wachezaji soka wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja kujitangaza.

Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Uingereza, Greg Clarke ameiambia kamati ya wabunge kwamba anahofia wachezaji watakabiliwa na matusi kutoka kwa mashabiki.

Lakini Chris Sutton anasema kuwa matamshi ya Clarke yataonyesha kuwa soka haliko tayari kwa wachezaji wa mapenzi ya jinsia moja.

“Baada ya mchezaji wa kwanza wa mapenzi ya jinsia moja kujitangaza wengine watafuata,” alisema katika taarifa aliyoiandika katika gazeti la Daily Mail.


Sutton mwenye umri wa miaka 43 aliongezea: “Hakuna muda mzuri kama sasa kwa wachezaji kujitangaza na kusema mimi ni mpenzi wa jinsia moja.”

No comments