CRISTIANO RONALDO AGEUKA MUOKOTA MIPIRA UWANJANI KATIKA TIMU YA MWANAWE

HAKUNA ubishi kwamba Cristiano Ronaldo ni baba anayejitoa kikamilifu katika malezi ya mwanawe, hivyo si jambo la kushangaa kumuona nyota huyo wa Real Madrid akihudhuria mechi ya kwanza Cristiano Jr ya timu yake ya U-8.

Mtoto huyo ambaye aliichezea timu yake ya Upozuelo dhidi ya Carrascal katika mechi ya wachezaji saba kila upande Ijumaa, alifunga goli huku Ronaldo akishuhudia kutokea nje ya uwanja pamoja na wazazi wa watoto wengine.

Ronaldo mwenyewe alihusika katika mechi hiyo pale alipochukua majukumu ya “ball boy” kufuatia shuti lililoenda nje ya mlango na akaenda kuuokota mpira na kuurudisha uwanjani mara kadhaa.


Pozuelo walishinda 4-3 kabla ya Roonaldo mwenyewe kushindwa kufunga siku mbili baadae pale Real Madrid waliposhikiliwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya Eibar.

No comments