CRISTIANO RONALDO ASEMA HANA MPANGO WA KUSTAAFU SOKA

STRAIKA Cristiano Ronaldo amesema kwamba kwa sasa hana mpango wa kustaafu kucheza soka na madala yake amepanga kujiweka fiti zaidi ili aweze kucheza miaka mingine kumi.

Staa huyo wa timu ya Real Madrid ameweza kutamba akiwa katika nchi za England na Hispania kipindi chote cha kibarua chake na pia ameweza kuwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Baada ya kufunga mabao 118 katika mechi 291 alizoichezea Manchester United nyota huyo wa timu ya taifa ya Ureno ameweza pia kufunga mabao 367 katika mechi 354 alizokichezea kikosi chake cha mjini Madrid.

Katika kazi yake nyota huyo ameweza kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu England moja la La Liga na la Ligi ya Mabingwa na kisha akaongeza jingine la mataifa akiwa na timu ya taifa ya Ureno.

Pamoja na mafanikio hayo, straika huyo ameonekana kutokuwa na mpango wa kuachana na soka baada ya kusema kuwa mipango yake ni kucheza kwa muda wa muongo mmoja mwingine.


“Maisha sio kuhusu soka,” alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 wakati akifungua hoteli yake mpya mjini Lisbon.

No comments