CRISTIANO RONALDO ATAJWA KIKOSI CHA TAIFA URENO KITAKACHOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2018

STAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Ureno kitakachocheza michezo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.

Ronaldo amerudi kwenye klabu yake baada ya kupona majeraha ya goti na amejumuishwa kwenye kikosi hicho kilichotwaa taji la michuano ya Euro 2016.


Ureno watakuwa nyumbani Oktoba 7, kuwakaribisha Andorra na baadae wataelekea visiwa vya Faroe.

No comments