Habari

DANNY ROSE ADAI ALAN SHEARER ALIKUWA SAHIHI KUSEMA UINGEREZA INATAPATAPA

on

BEKI wa kushoto wa timu ya
taifa ya Uingereza, Danny Rose amesema Alan Shearer alikuwa sahihi kusema kuwa
timu hiyo ya taifa itapatapa baada ya kujiuzulu kwa meneja Sam Allardyce.
Anasema kuwa sio jambo zuri kwa
meneja kuondoka muda mfupi akiwa bado hajatimiza mikakati aliyojiwekea na hilo
linaathiri pia wachezaji.
Rose alikuwa katika kikosi cha
Uingereza kilichofunga Slovakia katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia
chini ya uongozi wa Sam Allardyce.
“Nilimtumia ujumbe nikimshukuru
kwa kunijumuisha katika kikosi chake na kunifanya kuwa na heshima nyingine
katika ulingo wa soka la kimataifa. Nikamwambia pole sana kwa kupoteza nafasi
yake na kumtakia kila la kheri mbeleni,” alisema Rose.

Allardyce ameingia katika
historia ya kukaa kwa muda mfupi katika timu hiyo kwa sku 67 tu, aliingia baada
ya Roy Hodgson kubwaga manyanga alipotolewa mapema katika michuano ya Euro
2016.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *