DAVINA WA BONGOMUVI AFUNGUKA KUHUSU MASLAHI… asema wasanii wanaotegemea filamu pekee “imekula kwao”

STAA wa Bongomuvi, Halima Yahya “Davina” amesema kuwa njia pekee itakayowainua wasanii kimaisha ni kutafuta mtaji na kujitosa kwenye biashara mbalimbali ili kujiongezea kipato badala ya kutegemea filamu pekee.

Davina alisema kuwa wasanii ambao wamegundua ugumu wa maisha kwenye Bongomuvi, walijiongeza mapema kwa kujiingiza kwenye biashara ingawa pia kuna changamoto.

Alisema kuwa soko la filamu linazidi kushuka na hakuna dalili ya kulinyanyu, ndio maana ameamua kuwashauri wale ambao hawalioni hilo washituke na kuchukua hatua haraka.


Alisema kuwa, yeye kwa sasa anafanya biashara ya nguo za kike na bidhaa nyingine ambazo amekuwa akizifuata nje na kuziuza nchini.

No comments