Habari

DEMU AMPONZA MCHEZAJI NEW ZEALAND… apigwa marufuku kucheza mchezo mmoja baada ya kuingia nae msalani

on

MCHEZAJI wa timu ya Raga ya New
Zealand, Aaron Smith amepigwa marufuku kucheza mchezo mmoja baada ya kuingia
msalani na mwanamke katika uwanja wa ndege mjini Christchurch.
Hiyo ni kinyume na kanuni za
timu hiyo ya taifa.
Atakosa mchezo wa ubingwa wa
Raga dhidi ya Afrika Kusini mjini Durban.
Kocha wa All Bracks, Steve
Hansen amesema Smith mwenyewe amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Hansen ameongeza kwamba
mchezaji huyo wa miaka 27 anahisi kwamba ameivunja moyo timu yake, familia yake
na mpenzi wake.
“Ameomba kwenda nyumbani
kushughulikia masuala ya kibinafsi ambayo yameibuka kutokana na kisa hicho na
tuna furaha kumsaidia katika hilo,” amesema Hansen.
Kocha huyo amesema adhabu hiyo
iliafikiwa na kundi la viongozi wa timu ambalo lilijumuisha wachezaji.
Smith amechezea New Zealand
mashindano 54 tangu aanze kuwachezea mwaka 2012. Baadae mwaka 2012 alizuiwa
kucheza kwa muda kwa kuvunja amri ya kutotoka nje.

Mwaka 2014 alituma picha yake
ya utupu kwenye snapchat ambayo ilisambaa sana mitandaoni.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *