DIAMOND AJITETEA KUHUSU KUURUDIA WIMBO "MARIA SALOME" WA SAIDA KAROLI... asema mtindo huo upo ulimwenguni kote

DIAMOND Platnumz amesema kuwa mtindo wa kurudia nyimbo ambazo zilishawahi kuimbwa na wasanii wengine ni jambo la kawaida ilimradi taratibu zimefuatwa, zikiwemo za kukubaliana na mwenye wimbo.

Alisema kuwa tangu wimbo wake wa “Salome” utoke, wapo watu ambao wamekuwa wakimshangaa na kuonyesha kutofurahishwa na hatua yake hiyo bila kujua kwamba hilo ni jambo la kawaida.

“Mtindo wa msanii kurudia wimbo wa msanii wa kitambo upo ulimwenguni kote na hata hapa Bongo upo, ndio maana MwanaFA aliwahi kurudia wimbo “Ya Laiti” wa marehemu Bi Kidude, Ali Kiba alirudia wimbo wa Issa Matona, Ben Pol nae aliwahi kurudia wimbo wa Les Wanyika na Lady Jaydee aliimba “Siwema”,” alisema Diamond kupitia kwa meneja wake, Sallam Sharaff.


Diamond ameimba wimbo wa “Maria Salome” wa Saida Karoli uliotamba mwanzoni mwa mwaka 2000 na sasa ameupa jina la “Salome” na tyari umevutia watu wengi pengine kuliko nyimbo zilizotangulia kuigwa na wasanii wengine kabla yake.

No comments