DIAMOND AMPIGIA DEBE ALI KIBA TUZO YA MTV EMMA

DIAMOND Platnumz amewataka watanzania kumpigia kura kwa wingi staa mwenzie wa Bongofleva, Ali Kiba ili tuzo ya MTV EMMA ije nyumbani.

Diamond amesema kuwa kama mwaka jana tulibeba tuzo mbili, basi tujitahidi kupiga kura kwa wingi ili isionekane Tanzania tumeshuka mwaka huu.


“Kaingia Ali hivyo tupige kura kwa sababu tukishindwa maanake Tanzania ndio imeshindwa, Justin Bibber alichukua tuzo nne mwaka jana na mie nikafuata nikachukua mbili, sasa tukiikosa hii tutaonekana tumefeli zaidi,” alisema.

No comments