DIAMOND: MAADILI YA VIDEO YA “SALOME” YANARUHUSU KUPIGWA KOKOTE DUNIANI

DIAMOND Platnumz amesema kuwa wimbo wake mpya wa “Salome” unafaa kupigwa katika yoyote kwa vile mavazi yake yamezingatia tamaduni za makabila mbalimbali ndani na nje ya nchi barani Afrika.

Mbali na hilo, wimbo huo unaendelea kujizolea mashabiki wengi ndani na nje ya nchi, hali inayoonyesha kuwa umetolewa katika wakati mwafaka na kuahidi kuendelea kuandaa vitu vikali zaidi.

Meneja wa msanii huyo, Babu Tale alisema video ya wimbo huo kutazamwa zaidi ya mara mil 5 ushahidi kwamba umekubalika.


“Kwa ujumla ni kwamba wimbo “Salome” unafaa kupigwa katika nchi yoyote kwani mavazi yake yamezingatia makabila mbalimbali ndani na nje ya nchi barani Afrika,” alisema.

No comments