DIAMOND PLATNUMZ AAGIZA VIFAA GHALI KUBORESHA "WASAFI STUDIO"

MKALI wa wimbo "Salome", Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya WCB ambayo tayari imeshaanza kufanya hits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chati mbalimbali za muziki nchini.

Mwimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais anayeshughulikia Muungano na mazingira Januari Makamba na kumweleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.

“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwa hatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe oda watutengenezee,” alisema Diamond.

“Zingekuwa ni zile ndogondogo wangenipa lakini kwa sababu ni kubwa sana lazima utoe oda, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu.”


Pia waziri Makamba alimsifia produza wa Wasafi Records Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond, Salome ambao kwa sasa unafanya vizuri.

No comments