DIAMOND PLATNUMZ AFICHUA MAPENZI YAKE KWA BARNABA CLASSIC

MKALI wa muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platnumz ameweka wazi hisia zake na kudai kuwa msanii aliyekuwa akivutia hapa nchini enzi na enzi na bado anavutia na kupendwa kwa kazi zake ni Barnaba Classic.

Akizungumzia hilo, Diamond ameweka wazi kuwa ni msanii pekee aliyekuwa akimuiga na kuvutiwa na kazi zake kutokana na umahiri wa uimbaji wake.


Ameongeza kuwa baada ya kuanza jina katika muziki, ilibidi aanze kutafuta mtindo wake wa muziki ili kuepusha kuwachanganya mashabiki wao.

No comments