Habari

DIEGO ALVES AWAONYA MABEKI WAKE KUWA MAKINI NA KUTOFANYA MAKOSA

on

MLINDA mlango wa timu ya
Valencia, Diego Alves amewaonya mabeki wake akiwaeleza kuwa wanatakiwa kuwa
makini kutofanya makosa wanapokuwa katika eneo la hatari ya kuwa na rekodi
nzuri ya kuokoa mikwaju ya penati.
Mbrazil huyo alishindwa kuokoa
mkwaju wa penati uliochongwa na Los Che katika mchezo waliofungwa mabao 2-0
dhidi ya Atletico Madrid kabla ya mechi za kupisha za timu za taifa licha ya kuwa
alishaokoa zilizopigwa na Antoine Griezmann na Gabi.
Kwa kuokoa mikwaju hiyo
imemuongezea rekodi katika michuano ya La Liga ambapo hadi sasa ameokoa mikwaju
19 kati ya 37 aliyokutana nayo.
Baada ya kufanya vibaya
mwanzoni mwa msimu huu, Valencia kwa sasa inashika nafasi ya 19 na kesho kutwa anasafiri kwenda kuivaa Sporting Gijon kabla ya wiki moja baadae kwenda
kuwavaa mabingwa watetezi Barcelona mtanange ambao Alves anatarajia utakuwa ni
mgumu.
“Kucheza vibaya kunaweza
kubadili jinsi mchezaji anavyopiga penati,” Alves aliliambia gazeti la Marca.
“Lakini kila penati unayozuia
inakuoingezea majukumu ila nina matumaini hakutakuwepo na penati katika mechi
zijazo dhidi ya Barcelona.”
“Tangu nilipokuwa mdogo nilijikuta ikiwa ni rahisi kuzuia
mikwaju ya penati. Nina ujuzi mkubwa lakini bado siipendi hali hiyo kutokana
na kwamba mara nyingi huwa inanichanganya akili,” aliongeza nyota huyo.

Awali Alves alikuwa akihusishwa
kwenda kujiunga na Barcelona baada ya mlinda mlango Claudio Bravo kutimkia
Manchester City, lakini klabu hiyo ya Catalan ikaamua kumsajili Jasper
Cillessen.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *