DIEGO COSTA AONYWA AACHE UJEURI WA KUMKOROMEA KOCHA CONTE

DIEGO Costa ametakiwa kuwa makini na kuacha ujeuri, baada ya kukwaruzana na kocha wake, Antonio Conte.

Costa alimbwatukia Conte akitaka apumzishwe kipindi cha pili wakati wa mechi dhidi ya Leicester City Jumamosi iliyopita.

Nyota huyo wa Hispania pia aliwahi kukwaruzana na Jose Mourinho wakati kocha huyo akifundisha Chelsea.

Conte alisema Costa alitaka apumzishwe ili kuepuka kuonyeshwa kadi ya njano ambayo ingekuwa ya tano kwake msimu huu.

Kama angeonyeshwa kadi kwenye mchezo huo angeukosa mchezo wa Jumapili wiki hii dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Stanford Bridge, huku Mourinho akirejea kwa mara ya kwanza kwenye uwanja huo.

Mshambuliaji huyo wa Hispania alionekana kuchoshwa na kelele za kocha wake ambaye kila wakati alikuwa akisimama kumwelekeza jambo kutokana na kutoridhishwa na kiwango alichokionyesha.


Mourinho na Costa waliwahi kukwaruzana wakati wa Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Israel baada ya straika huyo kuchukizwa na maelekezo aliyopewa.

No comments