DIVOCK ORIGI ASEMA HAKERWI KUSUGULISHWA BENCHI LIVERPOOL

STRAIKA wa Liverpool, Divock Origi amedai kuwa hakerwi na kitendo cha kocha wake kumpiga benchi na badala yake anachokitaka ni ushindi wa timu.

Katika mechi saba za Ligi Kuu England, Origi ametokea benchi mara tano lakini hilo halimuumizi kichwa.


Fowadi huyo raia wa Ubelgiji amefunga katika michezo yote miwili aliyopewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

No comments