DOGO JANJA ASEMA AMEMPATA MTU "MWAFAKA" WA KUFUNGA NAE PINGU ZA MAISHA

RAPA Dogo Janja amesema amempata mtu sahihi ambaye anaweza kufunga  naye ndoa muda si mrefu ingawa hatua hiyo imeelezwa kuwa ni dharau kwa Madee, mlezi wake ambaye bado hajaoa.

“Kweli ninataka kuoa, muda si mrefu nitavuta jiko hivyo siwezi kusema ni lini ila suala hilo lipo kwenye mchakato,” alisema Dogo Janja alipohojiwa na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.


Wakati msanii huyo akisema hayo Madee ameshaweka wazi kwamba kitendo cha Dogo Janja kutaka kuoa kabla yake itakuwa kama dharau hivyo anapaswa kusubiri kwanza mpaka yeye afanye mambo ndipo atangaze ndoa.

No comments