DOKII: ACHENI WASANII WA FILAMU WAIGIZE UKAHABA, ULEVI MBONA POA TU

UMMY Wenceslaus “Dokii” anaamini kwamba msanii anapoigiza filamu inayohusu ulevi ama ukahaba, haina maana kwamba ndio tabia yake halisi bali ni kuvaa uhusika tu ambayo ni njia mojawapo ya kuonyesha athari ya matukio hayo.

“Msanii anapopewa nafasi ya kuigiza kama kahaba au mlevi ukiangalia imani yako inakuwa ngumu lakini ukiangalia majukumu yanayokuzunguuka ni lazima uigize keani una watoto wanahitaji ada, unatakiwa sadaka, kuigiza nafasi hizo si dhambi,” alisema Dokii.

Alisema: “Kuna wakati watu wanaweza kuhoji kuwa yule ameokoka kweli? Mbona anaigiza katika nafasi zile ambazo ni mbaya lakini wanasahau kuwa inawezekana ikawa ni sehemu ya uhubiri na hatupaswi kuwachukia walioangukia katika dhambi bali kuwaombea na kuwafundisha warudi katika njia iliyo sahihi.”


Dokii kwa sasa amestaafu uigizaji na kuelekea kazi ya Injili ingawa pia amekuwa akitoa ushauri kwa wasanii wa filamu wanaochipukia kwa lengo la kuigiza kwa ufanisi.

No comments