DOKII ASEMA KUWA CHANGAMOTO HAZIWEZI KUBADILI UOKOVU WAKE

MSANII wa filamu ambaye kwa sasa ameokoka, Dokii, amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, hawezi kubadili uamuzi wake wa kuanza kumtumikia Mungu.

Dokii alisema kuwa uamuzi wa kuokoka ni pamoja na kukabiliana na changamoto zilizomo kwenye wokovu ambazo baadhi yake ni kujitenga na mambo ambayo yanakwenda kinyume na mafundisho ya dini. 

“Kuna kazi kama kusherehesha kwenye shughuli mbalimbali na nyingine ambazo haziwezi kunikwaza, ninaweza kuzifanya kama kawaida, kama kuna mdau asihofie uokovu wangu,” alisema Dokii.

Mwigizaji huyo amesema kuwa ameamua kutoa ufafanuzi kwa sababu kuna baadhi ya wadau wamekuwa wakishindwa kutofautisha kazi ambazo mtu aliyeokoka anaweza kuzifanya kwa imani yake.


Alisema ni lazima aendelee kufanya baadhi ya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato cha kuendesha maisha yake ya kila siku.

No comments