DOMINIC SOLANKE ARIDHIA KUONGEZA MKATABA MPYA CHELSEA

KINDA anayetajwa kwamba atakuja kuwa mshambuliaji tishio katika Ligi Kuu ya Uingereza, Dominic Solanke amekubali kuongeza mkataba na klabu yake ya Chelsea.

Dominic mwenye umri wa miaka 19, anakaribia kuongeza mkataba mwingine na Chelsea baada ya kumalizika mazungumzo ya kupunguza mshahara wake.

Nyota huyo alikuwa anataka alipwe pauni 50,000 kwa wiki lakini matajiri wanaomiliki klabu hiyo wamemwambia kwamba anatakiwa kupunguza kiwango hicho kabla ya kupewa mkataba mpya.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times, mazungumzo kati ya mchezaji huyo na Chelsea yamefikia mahali pazuri na kwamba anaweza kukubali kulipwa nusu ya kima alichokuwa anataka.

Solanke ambaywe amecheza mechi moja tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu ya England mwaka huu alikuwa katika akademi ya timu hiyo ya watototrangu mwaka 2004.

Ingawa hajakuwa katika kiwango cha juu sana lakini baadhi ya wapenzi wa timu hiyo wanasema kwamba ni bonge la mshambuliaji aqmbaye atakuwa msaada mkubwa kwa Chelsea hapo baadaye.


“Kuna uwezekano wakaslipwa kiasi cha poauni 25,000 kwa wiki ambazo zinalimngan uwezo wakekwa sasa ingawaje najua kwamba baadac ya muda lazima Chelsea watamuongeza mshahara au kumuuza kwa pesa nyingi sana,” limeandika gazeti hilo.

No comments