DROGBA AMALIZANA NA MABOSI WAKE MONTREAL IMPACT

STAA Didier Drogba amekubali kuendelea kuichezea Montreal Impact baada ya kuzungumza na viungo wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa timu hiyo, Joey Saputo, wamemalizana na mpachikaji mabao huyo.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 38, aliripotiwa kukataa kuingia uwanjani katika mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Toronto.


Kocha wa Impact, Mauro Biello alisema Drogba alikasirika baada ya kuambiwa hatokuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.

No comments