DUDE ASEMA BONGOMUVI IMEINGILIWA NA WATU WASIO NA TAALUMA

DUDE amesema kuwa Bongomuvi imeingiliwa kwa madai kwamba kwa sasa mtu yeyote mwenye pesa akitaka kuwa maarufu anakimbilia huko na anakuwa mtayarishaji wa filamu ili mradi aonekane katika jamii.

Alisema kuwa mtindo huo unachangia kukwamisha filamu na kwamba umefika wakati wa kuanzisha vyombo makini vya kusimamia tasnia hiyo ili mtu akitaka kuingia Bongomuvi awe kama anaingia chuo kikuu kwa kuwa na kipaji cha uigizaji.

Dude ambaye jina lake halisi ni Kulwa Kikumba alisema kuwa bila ya wasanii kufanya mabadiliko soko la filamu nchini litaendelea kuporomoka na hatimaye kufa kabisa.


“Leo hii Diamond anafanikiwa kwasababu anafikiri zaidi hiyo ndiyo maana anaenda kimataifa lakini huku kwenye filamu kumeingiliwa, leo hii mtu yeyote mwenye pesa akitaka kuwa maarufu tu anakimbilia huku,” alisema.

No comments