DUDUBAYA ASEMA HAKUNA NJIA YA MKATO YA KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

RAPA mkongwe, Godfrey Tumaini “Dudubaya” amesema hakuna njia ya mkato ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya bila mhusika kuamua kwa dhati na kusutwa na dhamira kutoka moyoni.

“Kama una mtoto ambaye ni changudoa, hata ufanye nini kama dhamira yake haijamsuta na akaamua kwa dhati kutoka moyoni mwake, hataacha. Atakuwa anaruka hadi ukuta. Ndivyo ilivyo kwa watu ambao wameshajiingiza katika dawa za kulevya,” alisema Dudubaya.

Alisema, msanii mwenzake, Chid Beenz na wasanii wengine kama Ray C, hawawezi kuacha kutumia dawa za kulevya kwa watu kuwapeleka popote kama dhamira zao hazijawasuta kuhusu jambo hilo.

Wakati Dudubaya akisema hayo, Chid Beenz nae ameshatoa msimamo wake kuwa, hajali watu kusema kwamba amerudia dawa za kulevya, kwavile mashabiki wake hawajali hilo bali wanataka kazi.


Chid Beenz alifunguka kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusisitiza kuwa hawezi kuharibu kazi yake hata kidogo na kwamba atumie dawa hizo ama asitumie, hatakosea kufanya kile ambacho kimemweka matawi ya juu.

No comments