DULLY SYKES ASEMA HAKUNA MSANII WA BONGOFLEVA ANAYEMBABAISHA

MWIMBAJI Dully Sykes amedai hakuna msanii wa kisasa wala wa zamani anayemlingia ama kumvimbia kwasababu yeye anaheshimika na hajawahi kuchuja wala kushuka kwenye muziki hata siku moja.

Dully alisema hana tabia ya kuwafuatafuata vijana aliowasaidia kwenye muziki ila anamshukuru Mungu wengi waliofanikiwa humkumbuka na kumpa heshima yake.

“Hakuna kijana wangu wala mtoto yeyote niliyemsaidia kwenye muziki anayenivimbia ama kuniringia, wananiheshimu sana,” Dully alisema.

Mkali huyo amemtaja Naseeb Abdul “Diamond Platnumz” kuwa ndiye msanii anayemwonyesha nidhamu na kumweshimu zaidi kuliko wote aliowahi kuwasaidia.

“Watu wanalalamikaga ooh namsifia sana Diamond, nisiongee uongo, nakubali wote wananiheshimu lakini Diamond ananiheshimu na kunionyesha nidhamu zaidi.”


“Upendo anaonionyesha kati ya watoto niliowasaidia ni Diamond, Chid Mapenz alituletea viatu tukaenda kuchukua, wakati tunatoka watu kibao walikuja kutuangalia lakini kufika pale kamba ya kiatu changu ikawa kama inapwelea hivi, Diamond aliinama mbele za watu na kunifunga kamba, kwanini nisimzungumzie vizuri,” alifunguka zaidi Dully.

No comments