ESTER KIAMA: KAMA SI DUDE FILAMU YANGU YA "NGOMA NZITO" INGEBUMA

MWIGIZAJI wa Bongomuvi, Ester Kiama amesema kuwa bila ya msaada na maelekezo ya msanii mwezake Dude filamu yake mpya iitwayo "Ngoma Nzito" ingebuma.

“Kama ningekuwa peke yangu labda ingekuwa kazi ngumu sana kutengeneza filamu ya "Ngoma Nzito" ambayo ni nzuri na bora zaidi, Dude ni meneja sahihi kwangu amenishauri vizuri kikazi na msaada mkubwa kwangu,” alisema Ester.

Msanii huyo alisema hayo kufuatia kuwapo kwa uvumi kwamba wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini Ester akafafanua kuwa hizo ni hisia tu za  watu na kwamba ukaribu wake na Dude ni wa kikazi tu.


Ester alisema kuwa wakati anaandaa filamu hiyo alitumia wasanii wengi ambao bila kuwepo Dude wangemsumbua na asingefanikiwa kwa kiwango kinachotakiwa.

No comments