ESTER KIAMA WA BONGOMUVI AJINASIBU KUTIKISA KWENYE FILAMU

MSANII anayechipukia katika filamu, Ester Kiama amesema kuwa nyota yake inaendelea kung’ara ndani ya Bongomuvi na ana uhakika jina lake litakuwa kubwa.

“Anayetaka kuamini ninachokisema asipitwe na filamu ya “Ngoma Ngumu” aone jinsi nilivyoitendea haki na wasanii wengine wakongwe wakiwemo Dude, Baba Haji na Irene Uwoya,” alisema Kiama.

Alisema kuwa, mkongwe wa filamu Jacob Stephen “JB” amechangia kumtengeneza ili awe nyota wa baadae kwenye Bongomuvi na hataki kumwangusha katika hilo kwani pia anapenda kuigiza.


Alisema, kushiriki kwenye filamu ambayo ina wasanii wakongwe ni fahari kwake kwani anazidi kuongeza ujuzi kutoka kwao na kuutumia kikamilifu kwa manufaa yake.

No comments