FAIZA ALLY AWATAKA WASANII WA KIKE WACHAKARIKE WASITEGEMEE FILAMU PEKEE

MWIGIZAJI wa Bongo Movies Faiza Ally amesema kuwa kuna haja ya wasanii wa kike kuwa wabunifu kwa kutafuta shughuli za ziada za kufanya ili kujiongezea kipato badala ya kutegemea filamu peke yake.

Msanii huyo ambaye pia ni mwanamitindo alisema ametoa ushauri huo baada ya kuona soko la filamu sasa  linayumba.

“Kwa hali ilivyo sasa inawezekana wasanii wa kike wakajikuta kwenye mtego ambao utafanya wajihusishe na itendo vibaya kwa sababu tu ya kusaka fedha, ninawashauri wajiongeze mapema hali ni ngumu na soko la filamu limeshuka,” alisema Faiza.

Msanii huyo aliongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa kila kwenye macho hapaswi kuambiwa tazama na kutakiwa kujiimarisha kwa kufanya kazi nyingize tofauti na sanaa hiyo.

No comments