FEZA KESSY: VIDEO YA "WALETE" IMEFUNIKA ILE NILIYOFANYA NA CHEGGE

MREMBO wa Bongofleva, Feza Kessy ambaye pia aliwahi kushiriki shindano la Big Brother Africa amesema video ya wimbo wake mpya wa “Walete” imeifunika aliyofanya na Chegge.

Alisema kuwa tangu alipotoa wimbo wa “Sanuka” aliomshirikisha Chegge ilimchukua muda mrefu kuandaa wimbo mpya wa "Walete" kutokana na majukumu mengi aliyonayo kwa sasa.

“Kwenye muziki sina mzahaa huwa nina fanya kweli na hata video ya wimbo wa "Walete" ni kali na nina uhakika ni bora kuliko kunifanya na Chegge,” alisema Feza.


Alisema kuwa kama ilivyokuwa kwenye video ya "Sanuka", hata hiyo mpya imeongozwa na Hanscana na ameirekodi hapahapa nchini.

No comments