FM ACADEMIA KUJA NA NGOMA ZA UFUKWENI COCO JUMAPILI HII …Ijumaa wako Mango Garden


BENDI ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” Jumapili hii watakuwa kwenye ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam katika onyesho maalum.

Onyesho hilo ni la ufunguzi rasmi wa ukumbi mpya wa Coco Beach Letasi Lounge ambapo Ngwasuma litanguruma hapo kuanzia saa 10 alasiri hadi saa 6 za usiku.

Mbali na onyesho hilo, FM Academia watakuwepo Mango Garden Kinondoni Ijumaa kuadhimisha Nyerere Day.

Msemaji wa FM Academia Kelvin Mkinga ameiambia Saluti5 kuwa maonyesho yote mawili yatakuwa ni ya mseto wa nyimbo kali tupu mpya na za zamani.

No comments