FRANK RIBERY AJISAFISHA KUHUSU MADAI YA "UTUKUTU"

WINGA wa Bayern Munich, Frank Ribery amejitetea kuhusu tuhuma zinazodai kuwa ni mchezaji mkorofi akisema kwamba yeye sio mkorofi bali huwa anakuja juu pindi mchezaji anapojaribu kumjeruhi.

Msimu huu Mfaransa huyo ameshapamba vichwa vya habari katika mechi mbili tofauti baada ya kukwaruzana na nyota wenzake Felipe Melo, Felix Passiack na Nicolai Muller.

Hata hivyo pamoja na matukio hayo, Ribery anasisitiza kuwa kamwe hajawahi kuwa mkorofi uwanjani.

“Najifahamu mwenyewe kuwa natakiwa kuwa makini. Lakini nataka kuweka wazi kwamba mimi sio mchezaji mchafu,” mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliliambia jarida la Sport Blid.


“Wakati mwingine huwa napoteza utulivu lakini hii huwa inatokea wakati mchezaji mwingine anapojaribu kunijeruhi,” aliongeza staa huyo.

No comments