Habari

GABO ZIGAMBA AJISIFU UJANJA WA MJINI… anasema anang’ara kwavile anazijua fitina zote

on

GABO
Zigamba amesema kuwa yeye ni mjanja wa mjini na anazijua fitina zote ndio maana
nyota yake ndani ya Bongomuvi inazidi kung’ara kila uchao.
Alisema
kuwa maisha ya mjini ni lazima mtu ae mjanja vinginevyo anaweza kujikuta
anakimbia mji kwa sababu ya kukosa mbinu na ujanja wa kumwezesha kuendesha
maisha.
“Ninaposema
ujanja sina maana ya utapeli bali kujua mambo mengi yanayohusu maisha na jinsi
ya kuyafanyia kazi na sio kubweteka tu na kujikuta mambo yanakwenda vibaya,”
alisema.

Alisema
kuwa, msanii akiwa mjanja anaweza kuuza filamu zake mwenyewe na kupata kile kinacholingana
na jasho lake, lakini vinginevyo wajanja wachache watamdhulumu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *