GARETH SOUTHGATE AJIPONGEZA KUIONGOZA TIMU YA TAIFA ENGLAND

KAIMU kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate amesema alikuwa kwenye hatua muhimu kuchukua nafasi ya meneja wa zamani, Sam Allardyce. 

Southgate ambaye wakati wa uchezaji wake alikuwa beki awali, amekuwa akiinoa timu ya vijana chipukizi wenye umri chini ya miaka 21 na ataongoza klabu hiyo ya taifa ya Uingereza kwa michuano minane ijayo.


Allardyce aling’atuka siku ya Jumanne baada ya uchambuzi wa gazeti la Daily Telegraph kudai kuwa alitumia cheo chake kushiriki mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushauri kuhusu vile watu wangeweza “kukwepa” sheria za uhamiaji wakati wa kuhama kwa wachezaji.

No comments