GARY ATABIRI JOHN STONES KUICHEZEA ENGLAND MECHI 100

BEKI wa timu ya taifa ya England, Gary Cahill amesema kwamba anavyoamini staa mwenzake katika kikosi hicho John Stones ataweza kufikisha mechi 100.

Hadi sasa Stones mwenye umri wa miaka 22 tayari ameshacheza mechi 13 akiwa na timu hiyo ya taifa ya Englamnd na anavyoonekana atakuwa mhimili muhimu katikau siku zijazo.

Kutokana na hali hiyo, Cahili ambaye alishafikisha mechi ya 50 katika mchezo ambao walitoka sare na Slovenia, anasema kwamba anavyodhani beki huyo wa Manchester City ataweza kufikisha mechi 100 akiwa na timu hiyo ya Taifa.

“John ni mchezaji mahiri kutokana na kwamba nimewahi kucheza na mabeki wengi wa kati,” staa huyo aliliambia gazeti la Daily Mirror.


“Na kwa kuhamia Manchester City anakwenda kuwa chini ya ulinzi mzuri kutokana na kwamba atakuwa akicheza mechi kubwa ambazo zitamfanya aendelee kukuza kipaji chake,” aliongeza beki huyo mahiri.

No comments