GARY NEVILLE AMFAGILIA MOURINHO AKIAMINI ATAILETEA MAFANIKIO MANCHESTER UNITED

STAA wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amemfagilia kocha Jose Mourinho akisema chini yake anaamini ubingwa utapatikana.

Neville, mlinzi wa pembeni kulia ambaye reodi zinaonyesha anashika nafasi ya 17 kati ya wachezaji 50 bora zaidi kuwahi kuitumikia United, alisema kuwa Mourinho ameiboresha timu kwa kiasi kikubwa.

Alisema, hivi sasa wachezaji wanajiamini na wana morari ya ushindi katika ila mchezo, hivyo akipewa muda atairejeshea timu hiyo enzi za mataji ambayo yameadimika tangu kustaafu kwa Sir Alex Ferguson.

“Nimeiangalia timu kwa sasa inacheza vizuri na kwa malengo, imepunguza kupiga pasi nyingi, soka linavutia, inashambulia kwa nguvu na wachezaji wamerudi mchezoni na naona amerudisha kipaji cha Rooney,” alisema.

Neville ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, amesema anaamini Mreno huyo atampiku mtangulizi wake, Louis Van Gaal kwani tyari matunda ya usajili wake wa akili yanaonekana.

Nahodha huyo wa United mwaka 2007 aliwasihi mashabiki kumpa ushirikiano na kumvumilia Mourinho hata kma msimu huu hatatwaa ubingwa.


“Ingawa United hadi sasa ina pointi 16 ilizokuwa nazo wakati kama huu msimu uliopita, lakini Mourinho amempiku Van Gaal kwa mambo mengi, timu inaleta matumaini kila kukicha,” alisema.

No comments