GERARD PIQUE ASEMA VAN GAAL AMEMJENGEA UWEZO WA MAISHA YAKE KISOKA

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amempa tano Van Gal kuwa ni kati ya watu waliomjengea uwezo wa maisha yake ya kisoka.

Pique anaendelea kumweshimu Van Gal tangu akiwa katika majukumu ya kukinoa kikosi cha timu ya wakubwa ya timu ya taifa ya Hispania.

Amesema, kocha huyo ndiye aliyemfanya aongeze bidii kwa kumwambia wazi kwamba hakuwa tayari kumwamini kumpa namba katikakikosi cha wakubwa cha Barcelona.

Pique ameliambia gazeti la Daily Mail kwamba Van Gaal alimkatisha tamaa lakini kwakweli ndiye aliyemfanya kuwa mchezaji wa maana.

“Huwezi kujua nini kinaweza kukutokea. Unakuwa kwenye timu halafu kocha anakwambia wazi hufai. Van Gaal alinisukumia kwenye sakafu akaniambia sina nguvu na uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza cha Barcelona,” amesema.

“Ilikuwa kama pigo kwangu wakati ule. Katika Barcelona huwezi kwenda gym kuongeza utimamu wa mwili na nguvu mpaka ufike umri wa miaka 18. Ulikuwa wakati mgumu kwangu,” amesema.


Hata hivyo amesema kwamba changamoto hizo ambazo amepata kutoka kwa Van Gaal ndizo ambazo zimemfanya leo kuwa beki mkubwa na mwenye heshima kubwa duniuani.

No comments