GIANFRANCO ZOLAN AIWEKEA MATUMAINI CHELSEA YA ANTONIO CONTE

MWANASOKA wa zamani, Gianfranco Zolan amesema kuwa ana matumaini kuwa Chelsea msimu huu itapigania ubingwa ikiwa chini ya kocha wao mpya, Antonio Conte na huku akisema kuwa kwa kukosa michuano mikubwa ya Ulaya inaweza kuwa ni faida kubwa kwao.

Kwa sasa Chelsea inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointy 13 ilizoikusanya katika mechi saba na ipo nyuma kwa pointi dhidi ya vinara wanaoongoza Ligi hiyo Manchester City.

Pampoja na klabu hiyo ya Stamford Bridge kupewa nafasi lakini Zolan bado ana matumaini timu hiyo inaweza kushika kasi na kufanikiwa kutwaa taji hilo.

“Faida ni kwamba Chelsea hawashiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa,” Zola aliwaambia waandishi wa habari.


“Nadhani hilo linaweza kuwa jambo jema. Hii ni kutokana na kwa jinsi walivyobadirika. Ila nina uhakika,” aliongeza nyota huyo.

No comments