GIGGS PRESHA JUU ISHARA ZA UBINGWA LIVERPOOL

RYAN Giggs amebainisha kwamba anajisikia tumbo joto kila anapofikiria Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na anahofu kwamba msimu huu unaeza kuwa wao wa kutwa taji lao la kwanza katika miaka 27.

Liverpool wameanza vyema msimu huu na walikaa kileleni kwa kuifunga Crystal Palace juzi jioni.

Na hilo kwa Giggs, shabiki damu wa Manchester United ambaye pia ni mchezaji wa mafanikio zaidi akitwaa taji la England mara 13 si jambo la kulifikiria.

“Uwezekano ni wa Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990, wasitarajie mimi kusema lolote jingine zaidi ya kwamba najisikia presha inapanda,” aliandika katika safu yake kwenye gazeti la Daily Telegraph.

“Zamani sana walitupa changamoto United kutufanya tupigane kuwafikia kutokana na wao kulitwaa Kombe hilo mara 18.”


“Miaka 20 baadae United imecharuka hadi kulitwaa mara 20 na hakuna mtu wa upande wangu anayetaka kuona wanarejea juu tena.”

No comments