GIGY MONEY ATETEA "TAKE ONE" YA ZAMARADI MKETEMA... aiomba TCRA kutoa nafasi nyingine kwa kipindi hicho

NYOTA wa kunengua katika video za muziki wa Bongofleva nchini, Gigy Money amekitetea kipindi cha “Take One” kinachorushwa na Televisheni ya Clouds chini ya mtangazaji Zamaradi Mketema na kusema kuwa kipindi hicho kina mafunzo.

Gigy aliyasema hayo mara baada ya kamati ya mahudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kukifungia kipindi hicho kwa muda wa miezi mitatu.


Gigy alisema kuwa mamlaka ina sheria na kanuni, anawaomba kutoa nafasi nyingine ili kipindi hicho kiendelee kurushwa kwani kipindi kimoja au viwili tu ndivyo vilivyoharibu dhamira ya kipindi.

No comments