GUARDIOLA AITOA MANCHESTER CITY MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU ENGLAND

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa bado hajaridhishwa na kiwango cha kikosi chake na anashangazwa na baadhi ya wadau wa soka duniani kuanza kuamini huenda msimu huu akafanikisha azma ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya England pamoja na Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Guardiola ambaye mwishoni mwa juma lililopita alikiongoza kikosi chake katika uwanja wa Old Trafford kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, amesema ni mapema nno kwa Manchester City kupewa matarajio hayo.

“Sikubaliani na matarajio ya wadau wengi wa soka kuhusu kikosi changu kuwa miongoni mwa wanaofikiriwa kuwa mabingwa kwa msimu huu, bado hatujawa sawasawa kama ninavyo taka.”


“Ni vigumu kwa msimu wa kwanza kufanya maajabu kama ya kutwaa ubingwa Ligi ngumu ya England pia katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya, kuna changamoto kubwa ya kuwepo kwa klabu zenye vikosi  vyenye uwezo mkuwa na zimekaa kwa muda mrefu tofauti na Man City ambayo kwa sasa inajitengeneza,” alisema Guardiola.

No comments