GUARDIOLA ASEMA BADO YUPOYUPO SANA TU MAN CITY

KOCHA Pep Guardiora ameweka wazi mipango yake ya kukaa muda mrefu Manchester City baada ya mkataba wake wa miaka mitatu kumalizika.

Kauli ya Mhispania huyo imekuja baada ya kuwa na mwanzo mzuri tangu aanze kibarua chake Man City kwa kushinda mechi 10 kati ya 11 alizokwishaiongoza timu hiyo.

Wakati jana wakiwa kileleni mwa Ligi kabla ya kuivaa Tottenham, Guardiola alisema kwamba sasa anayafurahia maisha akiwa na klabu hiyo ya etihad na akasema kuwa kuna uwezekano akakaa kwa muda mrefu.

“Nina furaha sana mahali hapa na wala kwa sasa siwazi kuhusu kukaa miaka mitatu tu,” alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 45.


“Wakati nilipoamua kuzipa mkono wa kwaheri timu za Barcelona na Bayern Munich, nilisema kuwa inatosha lakini kwa hapa ninavyoona ninaweza kukaa zaidi,” aliongeza kocha huyo.

No comments