HARMONIZE AWASHANGAA WANAOMSAKAMA KUWA ANAMUIGA DIAMOND PLATNUMZ

MMOJA wa wasanii ambao kiwango chake kiko juu katika muziki wa Kizazi Kipya “Harmonize” amesema kuwa kila msanii ana “role model” wake na kwamba anashangaa kusikia baadhi ya watu wakimsakama kuwa anamuiga bosi wake, Diamond Platnumz.

Harmonize alisema kuwa kumuiga mtu ni jambo la kawaida katika sanaa na haliwezi kuepukika.

“Mimi role model wangu ni Diamond Platnumz na ndio maana siku zote nimekuwa nikisema kuwa natamani kuwa kama yeye kwa kumiliki lebo ya wasanii kama sasa nilivyo katika lebo yake ya WCB,” alisema Harmonize.

Aliongeza kuwa sio yeye tu bali wapo wasanii wengi ambao wamekuwa wakiiga sauti za nyota ambao wameshafanikiwa kwenye sanaa hiyo lakini baadae wanaibuka na ubunifu wao na kusimama imara.


Alisema kuwa, asionekane kama anafanya jambo la ajabu katika muziki bali ni la kawaida na wataendelea kuibuka wasanii wengine zaidi ambao watafanya kama yeye.

No comments