HATIMAYE G FIVE MWAMWINGIZA STUDIO MWANAHAWA CHIPOLOPOLO …anashuka na kitu “Subira Haina Hasara”


KUNDI la G Five Modern Taarab limeingia studio kurekodi kibao chao kipya kitakachokwenda kwa jina la “Subira Haina Hasara”.

Wimbo huo utaimbwa na mmoja wa waimbaji bora kabisa wa kike Mwanahawa Ali Chipolopolo.

Mkurungenzi wa G Five, Hamis Slim ameiambia Saluti5 kuwa wimbo huo utakuwa hewani ndani ya siku chache zijazo na itakuwa ni kete yao ya kwanza katika maandalizi ya kusuka albam mpya.

“Subira Haina Hasira” umerekodiwa katika studio za Sound Crafters chini ya producer Enrico ambapo kinanda cha kwanza kimepigwa na Omar Kisila huku kinanda cha pili kikipapaswa na Dullah.

G Five wamekuja na mfumo mpya ambapo yatasikika magitaa matatu – solo ambalo limepigwa na Kisolo, rhythm likitenywa na Muddy Kidoti huku bass likikung’utwa na Hamad.

No comments